Zaburi 69:13-14
Zaburi 69:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini mimi nakuomba wewe, ee Mwenyezi-Mungu; nikubalie ombi langu wakati unaopenda, ee Mungu. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu. Wewe ni mkombozi wa kuaminika. Kwa msaada wako amini uniokoe nisizame katika matope; uniokoe na hao wanaonichukia, unisalimishe kutoka vilindi vya maji.
Zaburi 69:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe kutoka kwa wanaonichukia, Na kutoka katika vilindi vya maji.
Zaburi 69:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji.