Zaburi 67:1-7
Zaburi 67:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Utuonee huruma, ee Mungu, utubariki; utuelekezee uso wako kwa wema; dunia yote ipate kutambua njia yako, mataifa yote yajue nguvu yako ya kuokoa. Watu wote wakutukuze, ee Mungu; watu wote na wakusifu! Mataifa yote yafurahi na kuimba kwa furaha; maana wawahukumu watu kwa haki, na kuyaongoza mataifa duniani. Watu wote wakutukuze, ee Mungu; watu wote na wakusifu! Nchi imetoa mazao yake; Mungu, Mungu wetu, ametubariki. Mungu aendelee kutubariki. Watu wote duniani na wamche.
Zaburi 67:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake. Njia yake ijulikane duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki. Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.
Zaburi 67:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu na atufadhili na kutubariki, Na kutuangazia uso wake. Njia yake ijulike duniani, Wokovu wake katikati ya mataifa yote. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani. Watu na wakushukuru, Ee Mungu, Watu wote na wakushukuru. Nchi imetoa mazao yake MUNGU, Mungu wetu, ametubariki. Mungu atatubariki sisi; Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.
Zaburi 67:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mungu aturehemu na kutubariki, na kutuangazia nuru za uso wake, ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki. Mungu atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha yeye.