Zaburi 63:1-4
Zaburi 63:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, wewe u Mungu wangu, nami nakutafuta kwa moyo; roho yangu inakutamani kama mtu mwenye kiu; nina kiu kama nchi kavu isiyo na maji. Nimetaka kukuona patakatifuni pako, niione nguvu yako na utukufu wako. Fadhili zako ni bora kuliko maisha, nami nitakusifu kwa mdomo wangu. Nitakushukuru maisha yangu yote; nitainua mikono yangu na kukuomba.
Zaburi 63:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako. Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Zaburi 63:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako. Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Zaburi 63:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji. Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na utukufu wako. Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakuadhimisha. Nitakusifu siku zote za maisha yangu, na kwa jina lako nitainua mikono yangu.