Zaburi 63:1-2
Zaburi 63:1-2 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka, mahali pasipo maji. Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na utukufu wako.
Zaburi 63:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, wewe u Mungu wangu, nami nakutafuta kwa moyo; roho yangu inakutamani kama mtu mwenye kiu; nina kiu kama nchi kavu isiyo na maji. Nimetaka kukuona patakatifuni pako, niione nguvu yako na utukufu wako.
Zaburi 63:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, Nafsi yangu inakuonea kiu, Mwili wangu wakuonea shauku, Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Zaburi 63:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)