Zaburi 53:1-3
Zaburi 53:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Ni wafisadi, na wametenda mambo ya kuchukiza, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu. Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
Zaburi 53:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu. Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
Zaburi 53:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa, hakuna hata mmoja atendaye mema. Mungu anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu. Kila mmoja amegeukia mbali, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja!
Zaburi 53:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu!” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema. Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni, aone kama kuna yeyote mwenye busara, kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu. Lakini wote wamekosa, wote wamepotoka pamoja, hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja.