Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 53

53
Kushutumiwa kwa Wasiomwamini Mungu
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Mahalathi. Utenzi wa Daudi.
1 # Rum 3:10-12; Zab 10:4 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;
Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza,
Hakuna atendaye mema.
2 # Zab 33:13; 2 Nya 15:2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu,
Aone kama yuko mtu mwenye akili,
Amtafutaye Mungu.
3 # Mhu 7:29 Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja,
Hakuna atendaye mema,
La! Hata mmoja.
4 # Yer 4:22 Je! Wafanyao maovu hawajui?
Walao watu wangu kama walavyo mkate,
Hawakumwita MUNGU.
5Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu,
Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru.
Umewatia aibu,
Kwa sababu MUNGU amewadharau.
6Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni!
MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake;
Yakobo atashangilia,
Israeli atafurahi.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 53: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha