Zaburi 51:3-5
Zaburi 51:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Nakiri kabisa makosa yangu, daima naiona waziwazi dhambi yangu. Nimekukosea wewe peke yako, nimetenda yaliyo mabaya mbele yako. Uamuzi wako ni wa haki hukumu yako haina lawama. Mimi ni mkosefu tangu kuzaliwa kwangu, mwenye dhambi tangu tumboni mwa mama yangu.
Zaburi 51:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu iko mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama, nikazaliwa nikiwa na hatia; Mama yangu akanichukua mimba nikiwa na dhambi.
Zaburi 51:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
Zaburi 51:3-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima. Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo, na kuwa na haki utoapo hukumu. Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.