Zaburi 40:1-2
Zaburi 40:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Nilimngojea Mwenyezi-Mungu kwa uvumilivu, akanielekea na kukisikia kilio changu. Aliniondoa katika shimo la hatari, alinitoa katika matope ya dimbwi, akanisimamisha salama juu ya mwamba, na kuziimarisha hatua zangu.
Zaburi 40:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nilimngoja BWANA kwa subira, Akaniinamia na kusikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
Zaburi 40:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nalimngoja BWANA kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu. Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.