Zaburi 39:4-5
Zaburi 39:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
“Ee Mwenyezi-Mungu, unijulishe mwisho wangu, siku zangu za kuishi zimenibakia ngapi, nijue yapitavyo kasi maisha yangu!” Kumbe umenipimia maisha mafupi sana! Maisha yangu si kitu mbele yako. Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!
Zaburi 39:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, unijulishe mwisho wangu, Na idadi ya siku zangu ni ngapi; Nijue jinsi maisha yangu yalivyo mafupi. Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
Zaburi 39:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, unijulishe mwisho wangu, Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani; Nijue jinsi nilivyo dhaifu. Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri; Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako. Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
Zaburi 39:4-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Ee BWANA, nijulishe mwisho wa maisha yangu na hesabu ya siku zangu; nijalie kujua jinsi maisha yangu yanavyopita upesi. Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi; muda wangu wa kuishi ni kama hauna thamani kwako. Maisha ya kila mwanadamu ni kama pumzi.