Zaburi 38:6-10
Zaburi 38:6-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimejipinda na kuinama sana, Mchana kutwa ninaenda nikiomboleza. Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu. Nimedhoofika na kupondeka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Moyo wangu unadundadunda, Nguvu zangu zimenitoka; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.
Zaburi 38:6-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimepindika na kuinama sana, Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika. Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu. Nimedhoofika na kuchubuka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.
Zaburi 38:6-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Nimepindika mpaka chini na kupondeka; mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Viungo vyangu vimeshambuliwa na homa; mwilini mwangu hamna nafuu yoyote. Nimelegea na kupondekapondeka; nasononeka kwa kusongwa moyoni. Ee Bwana, wewe wajua tazamio langu lote; kwako hakikufichika kilio changu. Moyo wanidunda, nguvu zimeniishia; hata macho yangu nayo yamekwisha fifia.
Zaburi 38:6-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu. Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. Ee BWANA, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako. Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza.