Zaburi 38:1-10
Zaburi 38:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Mishale yako imenichoma; mkono wako umenigandamiza. Hamna mahali nafuu mwilini mwangu, kwa sababu umenikasirikia; hamna penye afya hata mifupani mwangu, kwa sababu ya dhambi yangu. Nimefunikwa kabisa na dhambi zangu, zinanilemea kama mzigo mzito mno kwangu. Madonda yangu yameoza na kunuka, na hayo ni matokeo ya ujinga wangu. Nimepindika mpaka chini na kupondeka; mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Viungo vyangu vimeshambuliwa na homa; mwilini mwangu hamna nafuu yoyote. Nimelegea na kupondekapondeka; nasononeka kwa kusongwa moyoni. Ee Bwana, wewe wajua tazamio langu lote; kwako hakikufichika kilio changu. Moyo wanidunda, nguvu zimeniishia; hata macho yangu nayo yamekwisha fifia.
Zaburi 38:1-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako. Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata. Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu. Maana dhambi zangu zimenifunika kichwa, Kama mzigo mzito zimenilemea mno. Majeraha yangu yananuka na kutunga usaha, Kwa sababu ya upumbavu wangu. Nimejipinda na kuinama sana, Mchana kutwa ninaenda nikiomboleza. Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu. Nimedhoofika na kupondeka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Moyo wangu unadundadunda, Nguvu zangu zimenitoka; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.
Zaburi 38:1-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako. Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata. Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu. Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa, Kama mzigo mzito zimenilemea mno. Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu. Nimepindika na kuinama sana, Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika. Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu. Nimedhoofika na kuchubuka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.
Zaburi 38:1-10 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenipiga. Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu. Maovu yangu yamenifunika kama mzigo mzito mno. Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu. Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu. Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako. Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza.