Zaburi 34:7-14
Zaburi 34:7-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Malaika wa BWANA hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa. Onjeni mwone kwamba BWANA ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia. Mcheni BWANA enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote. Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao BWANA hawatakosa kitu chochote kilicho chema. Njooni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha BWANA. Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema, basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo. Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.
Zaburi 34:7-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao, na kuwaokoa katika hatari. Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema. Heri mtu anayekimbilia usalama kwake. Mcheni Mwenyezi-Mungu enyi watakatifu wake; maana wenye kumcha hawatindikiwi na kitu. Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa; lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema. Njoni enyi vijana mkanisikilize, nami nitawafundisha kumcha Mwenyezi-Mungu. Je, watamani kufurahia maisha, kuishi maisha marefu na kufurahia mema? Basi, acha kusema mabaya, na kuepa kusema uongo. Jiepushe na uovu, utende mema; utafute amani na kuizingatia.
Zaburi 34:7-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Malaika wa BWANA huwazungukia, Wamchao na kuwaokoa. Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumainia. Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, Maana, wamchao hawapungukiwi kitu. Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema. Njoni, enyi wana, mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha BWANA. Ni nani atamaniye uzima na atakaye kuishi, Siku nyingi afurahie mema? Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila. Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.
Zaburi 34:7-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Malaika wa BWANA hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa. Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu. Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawatahitaji kitu cho chote kilicho chema. Njoni, enyi wana, mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha BWANA. Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima, Apendaye siku nyingi apate kuona mema? Uuzuie ulimi wako na mabaya, Na midomo yako na kusema hila. Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.