Zaburi 34:17-20
Zaburi 34:17-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Waadilifu wakimlilia Mwenyezi-Mungu yeye huwasikia, na kuwaokoa katika taabu zao zote. Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo; huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa. Mateso ya mwadilifu ni mengi, lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote. Huvilinda viungo vya mwili wake wote, hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.
Zaburi 34:17-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Walilia, naye BWANA akasikia, Akawaponya kutoka kwa taabu zao zote. BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na huwaokoa waliopondeka roho. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA kutoka kwayo yote. Huihifadhi mifupa yake yote, Usivunjike hata mmoja.
Zaburi 34:17-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Walilia, naye BWANA akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini BWANA humponya nayo yote. Huihifadhi mifupa yake yote, Haukuvunjika hata mmoja.
Zaburi 34:17-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wenye haki hulia, naye BWANA huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote. BWANA yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho. Mwenye haki ana mateso mengi, lakini BWANA humwokoa nayo yote, huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.