Zaburi 32:1-3
Zaburi 32:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri aliyesamehewa dhambi, Na kuondolewa makosa yake. Heri ambaye BWANA hamhesabii hatia, Na ambaye rohoni mwake hamna hila. Nilipokosa kuungama dhambi zangu, mifupa yangu ilipooza Kwa kulia kwangu mchana kutwa.
Zaburi 32:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila. Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa Kwa kuugua kwangu mchana kutwa.
Zaburi 32:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa. Heri mtu yule ambaye BWANA hamhesabii dhambi, na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu. Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.
Zaburi 32:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake, mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa. Heri mtu ambaye Mwenyezi-Mungu hamwekei hatia, mtu ambaye hana hila moyoni mwake. Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu, nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.