Zaburi 25:12-15
Zaburi 25:12-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Watafanikiwa maishani mwao; Na wazawa wao wataimiliki nchi. Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake. Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.
Zaburi 25:12-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ni nani basi, mtu yule anayemcha BWANA? Atamfundisha katika njia atakayoichagua kwa ajili yake. Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, nao wazao wake watairithi nchi. Siri ya BWANA iko kwa wale wamchao, yeye huwajulisha agano lake. Macho yangu humwelekea BWANA daima, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka mtego.
Zaburi 25:12-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi-Mungu atamfunza njia ya kufuata. Mtu wa namna hiyo atafanikiwa daima, na wazawa wake watamiliki nchi. Mwenyezi-Mungu ni rafiki ya wale wamchao; yeye huwajulisha hao agano lake. Namwangalia Mwenyezi-Mungu daima; yeye atainasua miguu yangu mtegoni.
Zaburi 25:12-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua. Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa; Wazao wake watairithi nchi. Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake. Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.