Zaburi 16:7-9
Zaburi 16:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Namsifu Mwenyezi-Mungu kwa kuniongoza, usiku dhamiri yangu yanionya. Namweka Mwenyezi-Mungu mbele yangu daima; yuko pamoja nami, wala sitatikisika. Kwa hiyo nitafurahi kwa moyo wote na kushangilia, nami nitakaa salama salimini.
Zaburi 16:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitamhimidi BWANA aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu umenifundisha usiku. Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa. Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nao utukufu wangu unashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Zaburi 16:7-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nitamsifu BWANA ambaye hunishauri, hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha. Nimemweka BWANA mbele yangu daima. Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume, sitatikisika. Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama
Zaburi 16:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitamhimidi BWANA aniongozaye, Wakati wa usiku pia moyo wangu hunishauri. Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa. Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.