Zaburi 131:2-3
Zaburi 131:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Ila nafsi yangu imetulia na kuwa na amani, kama mtoto mchanga alivyotulia na mama yake; ndivyo nafsi yangu ilivyo tulivu. Ee Israeli, umtumainie Mwenyezi-Mungu, tangu sasa na hata milele.
Zaburi 131:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa kunyonya Kifuani mwa mama yake; Roho yangu ni kama mtoto, Aliyeachishwa kunyonya. Ee Israeli, umtarajie BWANA, Tangu leo na hata milele.
Zaburi 131:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu. Ee Israeli, umtarajie BWANA, Tangu leo na hata milele.