Zaburi 119:33-40
Zaburi 119:33-40 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, unifundishe kutii masharti yako; nami nitayashika mpaka mwisho. Unieleweshe nipate kuishika sheria yako, niifuate kwa moyo wangu wote. Uniongoze katika njia ya amri zako, maana humo napata furaha yangu. Unipe ari ya kuzingatia maamuzi yako, na si kwa ajili ya kupata faida isiyofaa. Uniepushe, nisifuate mambo ya upuuzi; unioneshe njia yako, unipe uhai. Unitimizie mimi mtumishi wako ahadi yako; ahadi unayowapa wale wanaokuheshimu. Uniokoe na lawama ninazoogopa; maana maagizo yako ni mema. Natamani sana kuzitii kanuni zako; unijalie uhai maana wewe ni mwadilifu.
Zaburi 119:33-40 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, unifundishe njia ya amri zako, Nami nitaishika hadi mwisho. Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote. Uniendeshe katika mapito ya amri zako, Kwa maana nimependezwa nayo. Unielekeze moyo wangu katika shuhuda zako, Wala usiielekee tamaa. Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako. Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako, Iliyo ya wanaokucha. Uniondolee laumu niiogopayo, Maana hukumu zako ni njema. Tazama, nimeyatamani mausia yako, Unihuishe kwa haki yako.
Zaburi 119:33-40 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, unifundishe njia ya amri zako, Nami nitaishika hata mwisho. Unifahamishe nami nitaishika sheria yako, Naam, nitaitii kwa moyo wangu wote. Uniendeshe katika mapito ya maagizo yako, Kwa maana nimependezwa nayo. Unielekeze moyo wangu na shuhuda zako, Wala usiielekee tamaa. Unigeuze macho yangu nisitazame visivyofaa, Unihuishe katika njia yako. Umthibitishie mtumishi wako ahadi yako, Inayohusu kicho chako. Uniondolee laumu niiogopayo, Maana hukumu zako ni njema. Tazama, nimeyatamani mausia yako, Unihuishe kwa haki yako.
Zaburi 119:33-40 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, nifundishe kuyafuata maagizo yako, nami nitayashika mpaka mwisho. Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako na kuitii kwa moyo wangu wote. Niongoze kwenye njia ya amri zako, kwa kuwa huko napata furaha. Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako, na siyo kwenye mambo ya ubinafsi. Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. Mtimizie mtumishi wako ahadi yako, ili upate kuogopwa. Niondolee aibu ninayoiogopa, kwa kuwa sheria zako ni njema. Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako.