Zaburi 104:24-28
Zaburi 104:24-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai vidogo kwa vikubwa. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema
Zaburi 104:24-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, umetenda mambo mengi mno! Yote umeyafanya kwa hekima! Dunia imejaa viumbe vyako! Mbali kule iko bahari - kubwa na pana, ambamo kumejaa viumbe visivyohesabika, viumbe hai, vikubwa na vidogo. Ndimo zinamosafiri meli, na lile dude Lewiyathani uliloliumba licheze humo. Wote wanakungojea wewe, uwapatie chakula chao kwa wakati wake. Wanaokota chochote kile unachowapa; ukifumbua mkono wako wanashiba vinono.
Zaburi 104:24-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa viumbe wako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai wakubwa kwa wadogo. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo Lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema
Zaburi 104:24-28 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako. Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, uliyemuumba acheze ndani yake. Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake. Wakati unapowapa, wanakikusanya, unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema.