Zaburi 102:1-3
Zaburi 102:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu, na kilio changu kikufikie. Usijifiche mbali nami wakati wa taabu! Unitegee sikio lako, unijibu upesi wakati ninapokuomba! Siku zangu zapita kama moshi; mifupa yangu yaungua kama katika tanuri.
Zaburi 102:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie. Usinifiche uso wako siku ya shida yangu, Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi. Maana siku zangu zinatoweka kama moshi, Na mifupa yangu inateketea kama kinga.
Zaburi 102:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie. Usinifiche uso wako siku ya shida yangu, Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi. Maana siku zangu zinatoweka kama moshi, Na mifupa yangu inateketea kama kinga.
Zaburi 102:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. Usinifiche uso wako ninapokuwa katika shida. Unitegee sikio lako, ninapoita, unijibu kwa upesi. Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi, mifupa yangu inaungua kama kaa la moto.