Methali 7:1-5
Methali 7:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, yashike maneno yangu, zihifadhi kwako amri zangu. Zifuate amri zangu nawe utaishi; yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Yafunge vidoleni mwako; yaandike moyoni mwako. Iambie Hekima: “Wewe ni dada yangu”, na Busara “Wewe ni rafiki yangu”. Vitakulinda mbali na mwanamke mbaya, vitakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni.
Methali 7:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Mwambie hekima, Wewe ndiwe dada yangu; Mwite ufahamu jamaa yako mwandani. Wapate kukulinda na malaya, Na mwasherati akubembelezaye kwa maneno yake.
Methali 7:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke. Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.
Methali 7:1-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako. Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Yafunge katika vidole vyako; yaandike katika kibao cha moyo wako. Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” uite ufahamu jamaa yako; watakuepusha na mwanamke mzinzi, kutokana na mwanamke mpotovu na maneno yake ya kubembeleza.