Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 7

7
Tamaa za Uasherati
1Mwanangu, yashike maneno yangu,
Na kuziweka amri zangu akiba kwako.
2 # Law 18:5; Mit 4:4; Isa 55:3; Kum 32:10 Uzishike amri zangu ukaishi,
Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.
3 # Kum 6:8; Mit 3:3; Isa 30:8; Yer 17:1; 2 Kor 3:3 Zifunge katika vidole vyako;
Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu;
Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke.
5Wapate kukulinda na malaya,
Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.
6Maana katika dirisha la nyumba yangu
Nalichungulia katika shubaka yake;
7 # Mit 6:32 Nikaona katikati ya wajinga,
Nikamtambua miongoni mwa vijana,
Kijana mmoja asiyekuwa na akili,
8Akipita njiani karibu na pembe yake,
Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,
9 # Ayu 24:15 Wakati wa magharibi, wakati wa jioni,
Usiku wa manane, gizani.
10 # 1 Tim 2:9 Na tazama, mwanamke akamkuta,
Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;
11 # 1 Tim 5:13; Tit 2:5 Ana kelele, na ukaidi;
Miguu yake haikai nyumbani mwake.
12Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani,
Naye huotea kwenye pembe za kila njia.
13Basi akamshika, akambusu,
Akamwambia kwa uso usio na haya,
14Kwangu ziko sadaka za amani;
Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu;
15Ndiyo maana nikatoka nikulaki,
Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona.
16 # Isa 19:9 Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri,
Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari.
17Nimetia kitanda changu manukato,
Manemane na udi na mdalasini.
18Haya, na tushibe upendo hata asubuhi,
Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba.
19Maana mume wangu hayumo nyumbani,
Amekwenda safari ya mbali;
20Amechukua mfuko wa fedha mkononi;
Atarudi wakati wa mwezi mpevu.
21Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi,
Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
22Huyo akafuatana naye mara hiyo,
Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni;
Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu;
23Hata mshale umchome maini;
Kama ndege aendaye haraka mtegoni;
Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
24Basi, wanangu, nisikilizeni sasa,
Mkayaangalie maneno ya kinywa changu.
25Moyo wako usizielekee njia zake,
Wala usipotee katika mapito yake.
26 # Neh 13:26 Maana amewaangusha wengi waliojeruhi,
Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.
27 # Mit 2:18; 1 Kor 6:9,10; Ebr 13:4; Ufu 22:15 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu,
Hushuka mpaka vyumba vya mauti.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 7: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha