Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 30:15-33

Methali 30:15-33 Biblia Habari Njema (BHN)

Mruba anao binti wawili wasemao, “Nipe, nipe!” Kuna vitu vitatu ambavyo kamwe havishibi, naam, vitu vinne visivyosema, “Imetosha!” Kuzimu, tumbo la mwanamke lisilozaa, ardhi isiyoshiba maji, na moto usiosema, “Imetosha!” Kama mtu akimdhihaki baba yake, na kudharau utii kwa mama yake, kunguru wa bondeni watamdonoa macho, na kuliwa na tai. Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, naam, mambo manne nisiyoyaelewa: Njia ya tai angani, njia ya nyoka mwambani, njia ya meli baharini, na kinachomvuta mwanamume kwa mwanamke. Mwenendo wa mwanamke mwasherati ni hivi: Yeye hula, akajipangusa mdomo, na kusema, “Sijafanya kosa lolote!” Kuna mambo matatu ambayo huitetemesha dunia, naam, mambo manne ambayo haiwezi kuyastahimili: Mtumwa anayekuwa mfalme; mpumbavu anayeshiba chakula; mwanamke asiyependwa anayeolewa; na mjakazi achukuapo nafasi ya bibi yake. Kuna viumbe vinne vidogo sana duniani, lakini vina akili sana: Sisimizi: Wadudu wasio na nguvu, lakini hujihifadhia chakula wakati wa kiangazi; pelele: Wanyama wasio na uwezo, lakini hujitengenezea makao miambani; nzige: Hawana mfalme, lakini wote huenda pamoja kwa vikosi; mjusi: Waweza kumshika mkononi, lakini huingia katika ikulu. Kuna viumbe vitatu vyenye mwendo wa kupendeza, naam, kuna viumbe vinne vyenye mwendo mzuri; simba: Mnyama mwenye nguvu kuliko wote, wala hamwogopi mnyama mwingine yeyote; jogoo aendaye kwa maringo; tena beberu; na mfalme mbele ya watu wake. Kama umekuwa mpumbavu hata ukajisifu, au kama umekuwa unapanga maovu, chunga mdomo wako. Maana ukisukasuka maziwa utapata siagi, ukimpiga mtu pua atatoka damu; kadhalika kuchochea hasira huleta ugomvi.

Shirikisha
Soma Methali 30

Methali 30:15-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi! Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi! Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa, Na vifaranga vya tai watalila. Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu. Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana. Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu. Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia. Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula; Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake. Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari. Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi. Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme. Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri. Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote; Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki. Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako. Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.

Methali 30:15-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi! Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi! Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila. Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu. Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana. Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu. Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia. Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula; Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake. Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa joto. Kwanga ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi. Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme. Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri. Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hatishwi na mwingine yeyote yule; Jogoo anayetamba; na beberu; Na mfalme asimamaye mbele ya watu wake. Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako. Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.

Shirikisha
Soma Methali 30

Methali 30:15-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi! Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi! Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa, Na vifaranga vya tai watalila. Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu. Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana. Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu. Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia. Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula; Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake. Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana. Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari. Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba. Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi. Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme. Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri. Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote; Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki. Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako. Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.

Shirikisha
Soma Methali 30

Methali 30:15-33 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)

“Mruba anao binti wawili. Wao hulia daima: ‘Nipe! Nipe!’ “Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe, naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’: Ni kaburi, tumbo lisilozaa, nchi isiyoshiba maji kamwe, na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ “Jicho lile limdhihakilo baba, lile linalodharau kumtii mama, litang’olewa na kunguru wa bondeni, litaliwa na tai. “Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana, naam, vinne nisivyovielewa: Ni mwendo wa tai katika anga, mwendo wa nyoka juu ya mwamba, mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari, nao mwendo wa mtu pamoja na msichana. “Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi, hula akapangusa kinywa chake na kusema, ‘Sikufanya chochote kibaya.’ “Kwa mambo matatu nchi hutetemeka, naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia: mtumwa anapokuwa mfalme, mpumbavu anaposhiba chakula, mwanamke asiyependwa anapoolewa, na mjakazi anapochukua nafasi ya bibi yake. “Vitu vinne duniani vilivyo vidogo, lakini vina akili nyingi sana: Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi. Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo, hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba. Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi. Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, hata hivyo huonekana katika majumba ya wafalme. “Viko vitu vitatu ambavyo vinapendeza katika mwendo wao, naam, vinne ambavyo hutembea kwa mwendo wa madaha: simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama, wala haogopi chochote; jogoo atembeaye kwa maringo, pia beberu, na mfalme jeshi lake linapomzunguka. “Ikiwa umefanya upumbavu na ukajitukuza mwenyewe, au kama umepanga mabaya, basi funika mdomo wako kwa mkono wako. Kwa maana kama vile kusukasuka maziwa hutoa siagi, na pia kule kufinya pua hutoa damu, kadhalika kuchochea hasira huleta ugomvi.”

Shirikisha
Soma Methali 30