Methali 3:5-8
Methali 3:5-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako. Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu. Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako, na kiburudisho mifupani mwako.
Methali 3:5-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.
Methali 3:5-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.
Methali 3:5-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche BWANA ukajiepushe na uovu. Hii itakuletea afya mwilini mwako, na mafuta kwenye mifupa yako.