Methali 3:11-17
Methali 3:11-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA, Wala usione ni taabu kurudiwa naye. Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye. Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.
Methali 3:11-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwanangu, usiidharau adhabu ya BWANA na usichukie kukaripiwa naye, kwa sababu BWANA huwaadibisha wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye. Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu, kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye. Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume; katika mkono wake wa kushoto kuna utajiri na heshima. Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani.
Methali 3:11-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanangu, usidharau adhabu ya Mwenyezi-Mungu, wala usiudhike kwa maonyo yake; maana Mwenyezi-Mungu humwonya yule ampendaye, kama baba amwonyavyo mwanawe mpenzi. Heri mtu anayegundua hekima, mtu yule anayepata ufahamu. Hekima ni bora kuliko fedha, ina faida kuliko dhahabu. Hekima ina thamani kuliko johari, hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo. Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu; kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima. Njia zake ni za kupendeza, zote zaelekea kwenye amani.
Methali 3:11-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA, Wala usione ni taabu kurudiwa naye. Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye. Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.