Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 3:11-17

Mithali 3:11-17 NEN

Mwanangu, usiidharau adhabu ya BWANA na usichukie kukaripiwa naye, kwa sababu BWANA huwaadibisha wale awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye. Heri mtu yule aonaye hekima, mtu yule apataye ufahamu, kwa maana hekima ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi. Hekima ana thamani kuliko marijani; hakuna chochote unachokitamani kinachoweza kulinganishwa naye. Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume; katika mkono wake wa kushoto kuna utajiri na heshima. Njia zake zinapendeza, mapito yake yote ni amani.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mithali 3:11-17