Methali 29:9-15
Methali 29:9-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha. Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake. Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza. Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu. Maskini na mdhalimu hukutana pamoja; BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili. Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele. Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.
Methali 29:9-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani. Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu na hutafuta kumuua mtu mnyofu. Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia. Kama mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu. Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: BWANA hutia nuru macho yao wote wawili. Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote. Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo humwaibisha mama yake.
Methali 29:9-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenye hekima akibishana na mpumbavu, mpumbavu huwaka hasira na kucheka bila kutulia. Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia, lakini watu wema huyalinda maisha yake. Mpumbavu huonesha hasira yake wazi, lakini mwenye hekima huizuia na kuituliza. Mtawala akisikiliza mambo ya uongo, maofisa wake wote watakuwa waovu. Maskini na mkandamizaji wanafanana kwa kitu kimoja: Wote wawili wamepewa macho na Mwenyezi-Mungu. Mfalme anayewaamua maskini kwa haki, atauona utawala wake umeimarika milele. Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake.
Methali 29:9-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)