Methali 29:15-27
Methali 29:15-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake. Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao. Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi; yeye ataufurahisha moyo wako. Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu; heri mtu yule anayeshika sheria. Mtumwa haonyeki kwa maneno matupu, maana ingawa anayaelewa yeye hatayatii. Wamwona mtu apayukaye bila kufikiri? Mtu mpumbavu ni afadhali kuliko yeye. Ambembelezaye mtumwa wake tangu utoto, mwishowe mtumwa huyo atamrithi. Mwenye ghadhabu huchochea ugomvi, mtu wa hasira husababisha makosa mengi. Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe, lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima. Anayeshirikiana na mwizi anajidhuru mwenyewe; husikia laana ya aliyeonewa bila kusema neno. Kuwaogopa watu ni kujitega mwenyewe, lakini anayemtumaini Mwenyezi-Mungu yu salama. Wengi hupenda kujipendekeza kwa mtawala, hali mtu hupata haki yake kwa Mwenyezi-Mungu. Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu, naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu.
Methali 29:15-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako. Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria. Haitoshi mtumwa kuonywa kwa maneno; Maana ajapoyafahamu hataitika. Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye. Amwendekezaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe. Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana. Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. Mshiriki wa mwizi huichukia nafsi yake mwenyewe; Asikia maapizo, wala hana neno. Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama. Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
Methali 29:15-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako. Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria. Haitoshi mtumwa kuonywa kwa maneno; Maana ajapoyafahamu hataitika. Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye. Amtunduiaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe. Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana. Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. Mshiriki wa mwivi huichukia nafsi yake mwenyewe; Asikia maapizo, wala hana neno. Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama. Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
Methali 29:15-27 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto asiyeonywa humwaibisha mama yake. Waovu wanapostawi, dhambi huongezeka pia; lakini wenye haki wataliona anguko lao. Mkanye mwanao, naye atakupa amani; atakuletea furaha unayotamani. Mahali pasipo na ufunuo, watu huacha kujizuia, bali ana heri mtu yule anayeitii sheria. Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu, hata akielewa, hataitikia. Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye. Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, atamletea sikitiko mwishoni. Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, naye mtu mwenye hasira ya haraka hutenda dhambi nyingi. Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima. Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; huapishwa lakini hathubutu kushuhudia. Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye Mwenyezi Mungu atakuwa salama. Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki.