Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 29:15-27

Mit 29:15-27 SUV

Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako. Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria. Haitoshi mtumwa kuonywa kwa maneno; Maana ajapoyafahamu hataitika. Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye. Amtunduiaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe. Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana. Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. Mshiriki wa mwivi huichukia nafsi yake mwenyewe; Asikia maapizo, wala hana neno. Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama. Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.