Methali 28:15-28
Methali 28:15-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtawala mwovu anayewatawala maskini, ni kama simba angurumaye au dubu anayeshambulia. Mtawala asiye na akili ni mdhalimu mkatili; lakini achukiaye mali ya udanganyifu atatawala muda mrefu. Mtu anayelemewa na hatia ya kuua mtu, atakuwa mkimbizi mpaka kaburini; mtu yeyote na asijaribu kumzuia. Aishiye kwa unyofu atasalimishwa, lakini mdanganyifu ataanguka kabisa. Anayelima shamba lake atapata chakula kingi, bali anayefuata yasiyofaa atapata umaskini tele. Mtu mwaminifu atapata baraka tele, lakini mwenye pupa ya kuwa tajiri hataepa adhabu. Si vizuri kumbagua mtu; watu hufanya mabaya hata kwa kipande cha mkate. Mtu bahili hukimbilia mali, wala hajui kwamba ufukara utamjia. Amwonyaye mwenzake hatimaye hupata mema zaidi, kuliko yule anayembembeleza kwa maneno matamu. Anayeiba mali ya baba yake au mama yake, akasema si kosa, hana tofauti yoyote na wezi wengine. Mchoyo huchochea ugomvi, lakini anayemtegemea Mwenyezi-Mungu atafanikiwa. Anayetegemea akili yake mwenyewe ni mpumbavu; lakini anayeishi kwa hekima atakuwa salama. Aliye mkarimu kwa maskini hatatindikiwa kitu, lakini anayekataa kuwaangalia atalaaniwa kwa wingi. Waovu wakitawala watu hujificha, lakini wakiangamia, waadilifu huongezeka.
Methali 28:15-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini. Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake. Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie. Aendaye kwa unyofu ataokolewa; Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara. Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha. Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa. Kupendelea watu si kwema; Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate. Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjia. Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali; Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake. Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu. Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina; Bali amtumainiye BWANA ataneemeshwa. Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa. Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi. Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.
Methali 28:15-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini. Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake. Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie. Aendaye kwa unyofu ataokolewa; Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara. Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha. Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa. Kupendelea watu si kwema; Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate. Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjilia. Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali; Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake. Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu. Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina; Bali amtumainiye BWANA atawandishwa. Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa. Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi. Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.
Methali 28:15-28 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kama simba angurumaye au dubu ashambuliaye, ndivyo alivyo mtu mwovu anayetawala wanyonge. Mtawala dhalimu hana akili, bali yeye achukiaye mapato ya udhalimu atafurahia maisha marefu. Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua atakuwa mtoro hadi kufa; mtu yeyote asimsaidie. Yeye ambaye mwenendo wake hauna lawama hulindwa salama, bali yeye ambaye njia zake ni potovu ataanguka ghafula. Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yule afuataye mambo ya upuzi atakuwa na umaskini wa kumtosha. Mtu mwaminifu atabarikiwa sana, bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka hataacha kuadhibiwa. Kuonesha upendeleo si vizuri, hata hivyo mtu atafanya kosa kwa kipande cha mkate. Mtu mchoyo ana tamaa ya kupata utajiri, naye hana habari kuwa umaskini unamngojea. Yeye amkemeaye mtu mwishoni hupata kibali zaidi, kuliko mwenye maneno ya kusifu isivyostahili. Yeye amwibiaye babaye au mamaye na kusema, “Si kosa,” yeye ni mwenzi wa yule aharibuye. Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye Mwenyezi Mungu atafanikiwa. Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu, bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama. Yeye ampaye maskini hatapungukiwa na kitu chochote, bali yeye awafumbiaye maskini macho hupata laana nyingi. Wakati waovu wanatawala, watu huenda mafichoni, bali waovu wanapoangamia, wenye haki hufanikiwa.