Methali 16:3-5
Methali 16:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake; hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi. Kila mwenye kiburi ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; hakika mtu wa namna hiyo hataacha kuadhibiwa.
Methali 16:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu.
Methali 16:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu.
Methali 16:3-5 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mkabidhi Mwenyezi Mungu lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi Mungu hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi. Mwenyezi Mungu huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.