Methali 16:1-17
Methali 16:1-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Binadamu hupanga mipango yake, lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi-Mungu. Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa, lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu. Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake; hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi. Kila mwenye kiburi ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; hakika mtu wa namna hiyo hataacha kuadhibiwa. Kwa utii na uaminifu mtu huondolewa dhambi, kwa kumcha Mwenyezi-Mungu huepuka uovu. Mwenyezi-Mungu akipendezwa na mwenendo wa mtu, huwageuza hata adui zake kuwa marafiki. Afadhali mali kidogo kwa uadilifu, kuliko mapato mengi kwa udhalimu. Mtu aweza kufanya mipango yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake. Mfalme huamua kwa maongozi ya Mungu; anapotoa hukumu hakosei. Mwenyezi-Mungu hutaka kipimo na mizani halali; mawe yote mfukoni ya kupimia ni kazi yake. Ni chukizo kubwa wafalme kutenda uovu, maana msingi wa mamlaka yao ni haki. Mfalme hupendelea mtu asemaye kwa unyofu; humpenda mtu asemaye ukweli. Hasira ya mfalme ni kama mjumbe wa kifo; mtu mwenye busara ataituliza. Uso wa mfalme ukingaa kuna uhai; wema wake ni kama wingu la masika. Kupata hekima ni bora kuliko dhahabu; kupata akili ni chaguo bora kuliko fedha. Njia ya wanyofu huepukana na uovu; anayechunga njia yake huhifadhi maisha yake.
Methali 16:1-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye. Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake. Kukata maneno huwa katika midomo ya mfalme; Kinywa chake hakitakosa katika hukumu. Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya BWANA; Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake. Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki. Midomo ya haki ni furaha ya wafalme; Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa. Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti; Lakini mtu mwenye hekima ataituliza. Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme, Na fadhili zake ni kama wingu la masika. Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha. Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.
Methali 16:1-17 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa Mwenyezi Mungu. Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na Mwenyezi Mungu. Mkabidhi Mwenyezi Mungu lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi Mungu hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi. Mwenyezi Mungu huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa. Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha Mwenyezi Mungu mtu hujiepusha na ubaya. Njia za mtu zinapompendeza Mwenyezi Mungu, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani. Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Mwenyezi Mungu huelekeza hatua zake. Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu, wala kinywa chake hakipotoshi haki. Vipimo na mizani za halali hutoka kwa Mwenyezi Mungu; mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye. Wafalme huchukia sana kutenda maovu, kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kupitia haki. Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu; humthamini mtu asemaye kweli. Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti, bali mtu mwenye hekima ataituliza. Uso wa mfalme ung’aapo, inamaanisha uhai; upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli. Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, kuchagua ufahamu kuliko fedha! Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya; yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake.
Methali 16:1-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye. Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake. Kukata maneno huwa katika midomo ya mfalme; Kinywa chake hakitakosa katika hukumu. Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya BWANA; Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake. Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki. Midomo ya haki ni furaha ya wafalme; Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa. Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti; Lakini mtu mwenye hekima ataituliza. Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme, Na fadhili zake ni kama wingu la masika. Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha. Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.