Methali 11:1-3
Methali 11:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
Shirikisha
Soma Methali 11Methali 11:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini matumizi ya kipimo halali ni furaha kwake. Kiburi huandamana na fedheha, lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima. Unyofu wa watu wema huwaongoza, upotovu wa wenye hila huwaangamiza.
Shirikisha
Soma Methali 11Methali 11:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
Shirikisha
Soma Methali 11