Methali 11:1-14
Methali 11:1-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mizani ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele. Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu. Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Methali 11:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini matumizi ya kipimo halali ni furaha kwake. Kiburi huandamana na fedheha, lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima. Unyofu wa watu wema huwaongoza, upotovu wa wenye hila huwaangamiza. Utajiri haufai kitu siku ya ghadhabu, lakini uadilifu huokoa kutoka kifo. Uadilifu wa watu wanyofu huinyosha njia yao, lakini waovu huanguka kwa uovu wao wenyewe. Uadilifu wa wanyofu huwaokoa na hatari, lakini wafitini hunaswa kwa tamaa zao wenyewe. Mwovu akifa tumaini lake nalo hutoweka; tazamio la asiyemcha Mungu huishia patupu. Mtu mnyofu huokolewa katika shida, na mwovu huingia humo badala yake. Asiyemcha Mungu huangamiza wengine kwa mdomo wake, lakini mwadilifu huokolewa kwa maarifa yake. Waadilifu wakipata fanaka mji hushangilia, na waovu wakiangamia watu hupiga vigelegele. Mji hufanikishwa kwa baraka za wanyofu, lakini huangamizwa kwa mdomo wa waovu. Anayemdharau jirani yake hana akili, mtu mwenye busara hukaa kimya. Apitapitaye akichongea hutoa siri, lakini anayeaminika rohoni huficha siri. Pasipo na uongozi taifa huanguka, penye washauri wengi pana usalama.
Methali 11:1-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake linapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu wanapoangamia, watu hushangilia. Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu. Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. Mwenye udaku hupitapita akifunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Methali 11:1-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA huchukia sana mizani za udanganyifu, bali vipimo sahihi ni furaha yake. Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu, bali unyenyekevu huja na hekima. Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao. Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu, bali haki huokoa kutoka mautini. Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka, bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe. Haki ya wanyofu huwaokoa, bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya. Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka; yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu. Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu, naye mtu mwovu huingia humo badala yake. Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa. Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha. Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa, bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa. Mtu asiye na akili humdharau jirani yake, bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake. Masengenyo husaliti tumaini, bali mtu mwaminifu hutunza siri. Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka, bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.