Nehemia 7:1-2
Nehemia 7:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya ukuta kukamilika, malango yote kuwa tayari, na kuteuliwa kwa walinzi, waimbaji na Walawi, nilimteua ndugu yangu Hanani kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akishirikiana na Hanania aliyekuwa mkuu wa ngome katika Yerusalemu; kwa sababu alikuwa mtu wa kutegemewa na anayemcha sana Mungu, hapakuwapo mwingine aliyelingana naye
Nehemia 7:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa, baada ya ukuta kujengwa, na milango kuisimamishwa na kuweka mabawabu, waimbaji na Walawi, ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
Nehemia 7:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa, hapo ukuta ulipojengwa, na milango nimekwisha kuisimamisha, na mabawabu, na waimbaji, na Walawi, wamewekwa, ndipo nilimwagiza ndugu yangu, Hanani, pamoja na yule Hanania, jemadari wa ngome, kuwa na amri juu ya Yerusalemu; kwa maana alikuwa mtu mwaminifu huyo, na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
Nehemia 7:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine.