Nehemia 7
7
1 Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. 2 Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. 3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni
(Ezra 2:1-70)
4 Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. 5 Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:
6 Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 7 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):
Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:
8wazao wa Paroshi | 2,172 |
9wazao wa Shefatia | 372 |
10wazao wa Ara | 652 |
11wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) | 2,818 |
12wazao wa Elamu | 1,254 |
13wazao wa Zatu | 845 |
14wazao wa Zakai | 760 |
15wazao wa Binui | 648 |
16wazao wa Bebai | 628 |
17wazao wa Azgadi | 2,322 |
18wazao wa Adonikamu | 667 |
19wazao wa Bigwai | 2,067 |
20wazao wa Adini | 655 |
21wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) | 98 |
22wazao wa Hashumu | 328 |
23wazao wa Besai | 324 |
24wazao wa Harifu | 112 |
25wazao wa Gibeoni | 95 |
26watu wa Bethlehemu na Netofa | 188 |
27watu wa Anathothi | 128 |
28watu wa Beth-Azmawethi | 42 |
29watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi | 743 |
30watu wa Rama na Geba | 621 |
31watu wa Mikmashi | 122 |
32watu wa Betheli na Ai | 123 |
33watu wa Nebo | 52 |
34wazao wa Elamu | 1,254 |
35wazao wa Harimu | 320 |
36wazao wa Yeriko | 345 |
37wazao wa Lodi, Hadidi na Ono | 721 |
38wazao wa Senaa | 3,930 |
39 Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) | 973 |
40wazao wa Imeri | 1,052 |
41wazao wa Pashuri | 1,247 |
42wazao wa Harimu | 1,017 |
43Walawi:
wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia) | 74 |
44 Waimbaji:
wazao wa Asafu | 148 |
45 Mabawabu wa malango:
wazao waShalumu, Ateri, Talmoni,Akubu, Hatita na Shobai | 138 |
46 Watumishi wa Hekalu:#7:46 Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
47wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,
48wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,
49wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,
50wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,
51wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,
52wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,
53wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
55wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
56wazao wa Nesia na Hatifa.
57 Wazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,
58wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
59wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.
60Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni | 392 |
61 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
62wazao waDelaya, Tobia na Nekoda | 642 |
63 Na kutoka miongoni mwa makuhani:
wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
64Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 65 Kwa hiyo, mtawala#7:65 Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70). aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.#7:65 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
66Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245. 68Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245 69ngamia 435 na punda 6,720.
70 Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000#7:70 Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6. za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani. 71 Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu,#7:71 Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172. na mane 2,200#7:71 Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300. za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
72 Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.
73 Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.
Ezra Asoma Sheria
Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,
Iliyochaguliwa sasa
Nehemia 7: NEN
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.
Used with Permission. All Rights Reserved Worldwide.