Marko 13:14-37
Marko 13:14-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Yudea na wakimbilie milimani; na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo! Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi. Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe. Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo. Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki; kwa maana watajitokeza Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, ikiwezekana, hata hao wateule. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele. Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. Na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu. Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu; nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Lakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jogoo, au asubuhi; asije akawasili ghafla akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Marko 13:14-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo! Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi. Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe. Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo. Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki; kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele. Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu. Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu; nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Marko 13:14-37 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mtakapoona ‘Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake), hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani. Aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu. Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake. Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo! Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi. Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena. Kama Bwana asingepunguza siku hizo hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo. “Basi mtu akiwaambieni, ‘Tazama, Kristo yupo hapa,’ au ‘Yupo pale,’ msimsadiki. Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, kwa ajili ya kuwapotosha wateule wa Mungu kama ikiwezekana. Lakini nyinyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea. “Basi, siku hizo, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza. Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa. Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu. Kisha atawatuma malaika wake wawakusanye wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu. “Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa mavuno umekaribia. Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo hayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana. Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia. Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. “Lakini, juu ya siku au saa hiyo hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye. Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini. Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia na mlinzi wa mlango awe macho. Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi. Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala. Ninayowaambieni nyinyi, nawaambia wote: Kesheni!”
Marko 13:14-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Yudea na wakimbilie milimani; na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo! Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi. Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe. Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo. Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki; kwa maana watajitokeza Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, ikiwezekana, hata hao wateule. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele. Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. Na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu. Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu; nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Lakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jogoo, au asubuhi; asije akawasili ghafla akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Marko 13:14-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo! Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi. Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe. Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo. Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki; kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele. Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu. Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu; nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie. Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Marko 13:14-37 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
“Mtakapoona ‘chukizo la uharibifu’ limesimama mahali pasipolipasa (asomaye na afahamu), basi wale walio Yudea wakimbilie milimani. Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke au kuingia ndani ili kuchukua chochote. Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa baridi. Kwa maana siku hizo zitakuwa za dhiki kuu ambayo haijapata kuwa tangu mwanzo, hapo Mungu alipoumba ulimwengu, hadi leo, na wala haitakuwa tena kamwe. “Kama Mwenyezi Mungu hangefupisha siku hizo, kamwe hakuna mtu yeyote angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, wale aliowachagua, amezifupisha siku hizo. Wakati huo mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Al-Masihi huyu hapa!’ au, ‘Tazama, yuko kule,’ msisadiki. Kwa maana watatokea masihi wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule. Hivyo jihadharini. Nimekwisha kuwaambia mambo haya yote mapema kabla hayajatukia. “Lakini katika siku hizo, baada ya hiyo dhiki, “ ‘jua litatiwa giza nao mwezi hautatoa nuru yake; nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’ “Ndipo watu wote watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Naye atawatuma malaika wake wawakusanye wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka miisho ya dunia hadi miisho ya mbingu. “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. “Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake. Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia. Ni kama mtu anayesafiri. Anaiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwamuru yule bawabu aliye mlangoni akeshe. “Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko, akija ghafula asije akawakuta mmelala. Lile ninalowaambia ninyi, nawaambia watu wote: ‘Kesheni!’ ”