Marko 10:35-37
Marko 10:35-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakamwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lolote tutakalokuomba. Akawaambia, Mwataka niwafanyie nini? Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kulia, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako.
Marko 10:35-37 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakaja kwake na kumwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie lolote tutakalokuomba.” Naye akawaambia, “Je, mwataka niwafanyie jambo gani?” Wakamwambia, “Tupe kukaa mmoja upande wako wa kuume na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wako.”
Marko 10:35-37 Biblia Habari Njema (BHN)
Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” Yesu akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?” Wakamjibu, “Uturuhusu kuketi mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wako.”
Marko 10:35-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakamwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lo lote tutakalokuomba. Akawaambia, Mwataka niwafanyie nini? Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako.