Mathayo 5:44-45
Mathayo 5:44-45 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu nyinyi, ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu.
Mathayo 5:44-45 Swahili Revised Union Version (SRUV)
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Mathayo 5:44-45 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)