Mathayo 26:1-5
Mathayo 26:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, “Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe.” Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa, kuhani mkuu. Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue. Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.
Mathayo 26:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulubiwe. Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa; wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua. Lakini wakasema, Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia miongoni mwa watu.
Mathayo 26:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa Yesu alipomaliza maneno hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulibiwe. Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa; wakafanya shauri pamoja, ili wamkamate Yesu kwa hila na kumwua. Lakini wakasema, Isiwe wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia katika watu.
Mathayo 26:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yesu alipomaliza kusema hayo yote, akawaambia wanafunzi wake, “Kama mnavyojua, baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, naye Mwana wa Adamu atasalitiwa ili asulubiwe.” Basi viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakakusanyika katika jumba la utawala la kuhani mkuu, jina lake Kayafa. Wakapanga kumkamata Yesu kwa siri na kumuua. Lakini wakasema, “Isiwe wakati wa Sikukuu, kusitokee ghasia miongoni mwa watu.”