Walawi 25:35-37
Walawi 25:35-37 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kama ndugu yako amekuwa maskini hata asiweze kujitunza mwenyewe akiwa pamoja nawe, ni lazima umtunze aendelee kuishi nawe; mtendee kama mgeni au msafiri aliye kwako. Usimtake akulipe riba ya namna yoyote ile. Ila mche Mungu, naye ndugu yako apate kuishi pamoja nawe. Usimkopeshe fedha kwa riba au kumpa chakula ili akulipe faida.
Walawi 25:35-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe. Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida.
Walawi 25:35-37 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“ ‘Ikiwa mmoja wa wazawa wa nchi yako amekuwa maskini, naye akashindwa kujitegemeza mwenyewe katikati yako, msaidie kama vile ambavyo ungelimsaidia mgeni au kama mkazi wa muda, ili aweze kuendelea kuishi katikati yako. Usichukue riba wala faida yoyote kutoka kwake, bali utamwogopa Mungu wako, ili mzawa wa nchi yako aweze kuendelea kuishi katikati yako. Usimkopeshe fedha ili alipe na riba, wala usimuuzie chakula kwa faida.
Walawi 25:35-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)