Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo ya Walawi 25

25
Mwaka wa Sabato
1 # Kut 23:10-11 Kisha BWANA akanena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia, 2#Kut 23:10; Law 26:34,35; 2 Nya 36:21 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya BWANA. 3Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake; 4lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa BWANA; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu. 5#2 Fal 19:29; Isa 37:30 Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi. 6Na hiyo Sabato ya nchi itakuwa chakula kwenu; kwako wewe, na kwa mtumishi wako, na kwa mjakazi wako, na kwa mtumishi aliyeajiriwa, na kwa mgeni wako akaaye pamoja nawe; 7na kwa wanyama wako, na kwa wanyama walio katika nchi yako; mavuno yote yatakuwa ni chakula chao.
Mwaka wa Jubilii
8Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arubaini na tisa. 9#Law 23:24; 16:20,30 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. 10#Kut 20:2; Ezr 6:3; Isa 49:24,25; Yer 34:8,15,17; Lk 4:19; Gal 5:1; Hes 36:4 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kuwatangazia uhuru watu wote katika nchi; itakuwa ni mwaka wa jubilii#25:10 Kiasili, maana ya Jubilii ni baragumu iliyopigwa kila mwaka wa hamsini. kwenu; na kila mtu atairudia milki yake, na kila mtu atarejea kwa jamaa yake. 11Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni jubilii kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa. 12Kwa kuwa ni jubilii; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula mavuno yake yatokayo shambani. 13#Law 27:24; Hes 36:4 Mwaka huo wa jubilii mtairudia kila mtu milki yake. 14#Law 19:13; 1 Sam 12:3; Zab 10:18; Mik 2:2; 1 Kor 6:8 Tena kama ukimwuzia jirani yako chochote, au kununua chochote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; 15kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya jubilii, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe. 16Kama hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama hesabu yake ilivyo. 17#Mit 14:31; 22:22; Yer 7:6; Eze 22:29; 1 The 4:6 Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 18#Law 26:5; Kum 12:10; Zab 4:8; Mit 1:33; Yer 23:6 Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama. 19Nayo nchi itazaa matunda yake, nanyi mtakula na kushiba, na kuishi humo salama. 20#Mt 6:25; Hes 11:4-13; 2 Fal 6:15 Na kama mkisema, Je! Mwaka wa saba tutakula nini? Angalieni hatutapanda mbegu, wala kukusanya mavuno yetu; 21#Kut 16:29; Kum 28:8; Zab 33:12; 119:2; Mit 3:33; 8:32; 1 Tim 4:8 ndipo nitawaamria baraka yangu iwe juu yenu mwaka wa sita, nayo inchi itazaa matunda ya kutosha miaka mitatu. 22#2 Fal 19:29; Yos 5:11 Na mwaka wa nane mtapanda mbegu, na kuyala yale matunda, akiba hiyo ya zamani, hata mwaka wa tisa, hadi matunda yake yatakapoletwa ndani, mtakula hiyo akiba ya zamani. 23#Kum 32:43; 2 Nya 7:20; Zab 24:1; 85:1; Isa 8:8; Hos 9:3; Yoe 2:18; Zab 119:19; 1 Pet 2:11 Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wapangaji wangu. 24Nanyi mtatoa ukombozi kwa ajili ya nchi, katika eneo lote la milki yenu.
25 # Rut 2:20; 3:2 Ikiwa nduguyo amekuwa maskini, na kuuza sehemu ya milki yake, ndipo jamaa yake aliye karibu naye atakuja, naye ataikomboa ile aliyoiuza nduguye. 26Na kama mtu hana atakayeikomboa, naye mwenyewe amepata mali na kujiona kuwa anayo ya kutosha kuikomboa; 27ndipo na aihesabu hiyo miaka ya kuuzwa kwake, na kilichozidi kumrudishia huyo mtu aliyeinunua; naye atairejea milki yake. 28Lakini asipoweza kujipatia mwenyewe, ndipo hiyo iliyouzwa itakaa mkononi mwake huyo aliyeinunua, hadi mwaka wa jubilii; na katika jubilii ataliachilia, naye mwenyewe atairejea milki yake.
29Tena ikiwa mtu anauza nyumba ya kukaa, iliyo ndani ya mji wenye kuta, ndipo ana ruhusa kuikomboa katika mwaka mmoja mzima baada ya kuiuza; atakuwa na amri ya kuikomboa muda wa mwaka mzima. 30Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika jubilii. 31Lakini nyumba za vijiji, ambavyo havikuzingirwa na kuta, zitahesabiwa pamoja na mashamba ya nchi; nazo zina ruhusa ya kukombolewa, nazo zitatoka katika jubilii. 32#Yos 21:2 Pamoja na hayo, miji ya Walawi, nyumba za miji ya milki yao, Walawi wana ruhusa ya kuzikomboa majira yoyote. 33Tena mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa nyumba iliyouzwa na mji wa milki yake, itatoka katika jubilii; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli. 34#Mdo 4:36 Lakini konde la malisho ya miji yao lisiuzwe kwa kuwa ni milki yao ya daima.
35 # Kum 15:7-8; Zab 37:26; Mit 14:31; Lk 6:35; Mdo 11:29; Rum 12:18; 1 Yoh 3:17 Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. 36#Kut 22:25; Kum 23:19; Neh 5:7; Zab 15:5; Mit 28:8; Eze 18:8,13,17 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe. 37#Kut 22:25; Kum 23:19-20 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida. 38Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili niwape nchi ya Kanaani, nipate kuwa Mungu wenu.
39 # Kut 21:2-6; 22:3; Kum 15:12-18; 1 Fal 9:22; 2 Fal 4:1; Yer 34:14 Tena kwamba nduguyo amekuwa maskini pamoja nawe, akajiuza kwako; usimfanye akutumikie kama mtumwa; 40kwako wewe atakuwa mfano wa mtumishi aliyeajiriwa, au mfano wa msafiri; naye atatumika kwako hadi mwaka wa jubilii; 41ndipo atakapotoka kwako aende zake, yeye na wanawe pamoja naye, naye atairejea jamaa yake mwenyewe, tena atairejea milki ya baba zake. 42#Rum 6:22; 1 Kor 7:23 Kwa kuwa hao ni watumishi wangu, niliowaleta watoke nchi ya Misri; wasiuzwe kama watumwa. 43#Kut 1:13,14; 2:23; 3:7,9; 5:14; Isa 47:6; Efe 6:9; Kol 4:1; Kut 1:17,21; Kum 25:18; Mal 3:5 Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche Mungu wako. 44Tena kuhusu watumishi wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando yenu, katika hao mtanunua watumishi na wajakazi. 45Tena wana wa wageni wakaao kati yenu mtajinunulia, na katika jamaa zao walio pamoja nanyi, waliowazaa katika nchi yenu; wao watakuwa milki yenu. 46Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumishi wenu kwa hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli.
47Tena kama mgeni au mtu akaaye nawe akitajirika, na nduguyo amekuwa maskini karibu naye, akajiuza kwa huyo mgeni, au kwa huyo akaaye kwako, au kwa ukoo wa jamaa ya huyo mgeni; 48baada ya kuuzwa aweza kukombolewa; mtu mmoja miongoni mwa ndugu zake ana ruhusa kumkomboa; 49au mjomba wake, au mwana wa mjomba wake, ana ruhusa ya kumkomboa, au mtu yeyote aliye karibu naye wa jamaa yake, ana ruhusa ya kumkomboa; au kama yeye mwenyewe amepata mali, ana ruhusa ya kujikomboa mwenyewe. 50Naye atafanya hesabu na huyo aliyemnunua, tangu mwaka huo aliojiuza hata mwaka wa jubilii; na ile bei ya kuuzwa kwake itakuwa kama hesabu ya hiyo miaka ilivyo; atakuwa pamoja naye kama majira ya mtumishi aliyeajiriwa yalivyo. 51Ikiwa ingali imesalia miaka mingi, kama hesabu yake ilivyo ndivyo atakavyolipa bei ya ukombozi wake, katika hiyo fedha ambayo alinunuliwa kwayo. 52Tena kama imesalia miaka michache tu hadi mwaka wa jubilii, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake. 53Kama mtumishi aliyeajiriwa mwaka hadi mwaka, ndivyo atakavyokuwa pamoja naye; asitawale juu yake kwa nguvu mbele ya macho yako. 54Tena kwamba hakukombolewa kwa njia mojawapo ya hizi, ndipo atatoka katika mwaka wa jubilii, yeye, pamoja na watoto wake. 55Kwa kuwa wana wa Israeli ni watumishi; ni watumishi wangu niliowaleta watoke katika nchi ya Misri; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Iliyochaguliwa sasa

Mambo ya Walawi 25: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

Videos for Mambo ya Walawi 25