Maombolezo 3:20-23
Maombolezo 3:20-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu. Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.
Maombolezo 3:20-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Nayafikiria hayo daima, nayo roho yangu imejaa majonzi. Lakini nakumbuka jambo hili moja, nami ninalo tumaini: Kwamba fadhili za Mwenyezi-Mungu hazikomi, huruma zake hazina mwisho. Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno.
Maombolezo 3:20-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nafsi yangu ingali ikiyakumbuka hayo, Nayo imeinama ndani yangu. Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.
Maombolezo 3:20-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ninayakumbuka vyema, nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu. Hata hivyo najikumbusha neno hili na kwa hiyo ninalo tumaini. Kwa sababu ya upendo mkuu wa BWANA, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu.