Yobu 21:1-16
Yobu 21:1-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Yobu akajibu: “Sikilizeni kwa makini maneno yangu; na hiyo iwe ndiyo faraja yenu. Nivumilieni, nami nitasema, na nikisha sema endeleeni kunidhihaki. Je, mimi namlalamikia binadamu? Ya nini basi, nikose uvumilivu? Niangalieni, nanyi mshangae, fumbeni mdomo kwa mkono. Nikifikiri yaliyonipata nafadhaika nafa ganzi mwilini kwa hofu. Kwa nini basi waovu wanaishi bado? Mbona nguvu zao zaongezeka hata uzeeni? Huwaona watoto wao wakifanikiwa; na wazawa wao wakipata nguvu. Kwao kila kitu ni salama bila hofu; wala kiboko cha Mungu hakiwafikii. Naam, ng'ombe wao wote huongezeka, huzaa bila matatizo yoyote. Watoto wao wachanga huwatembeza kama kundi; na watoto wao hucheza ngoma; hucheza muziki wa ngoma na vinubi, na kufurahia sauti ya filimbi. Huishi maisha ya fanaka kisha hushuka kwa amani kuzimu. Humwambia Mungu, ‘Usitusumbue! Hatutaki kujua matakwa yako. Mungu Mwenye Nguvu ni nini hata tumtumikie? Tunapata faida gani tukimwomba dua?’ Kufanikiwa kwao si kuko mikononi mwao, wakiwa wamemweka Mungu mbali na mipango yao?
Yobu 21:1-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Yasikizeni sana maneno yangu; Jambo hili na liwe faraja yenu. Niacheni, nami pia nitanena; Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki. Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri? Niangalieni, mkastaajabu, Mkaweke mkono kinywani. Hata nikumbukapo nahuzunika, Na utisho wanishika mwilini mwangu. Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu? Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao. Nyumba zao ni salama bila hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi. Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng'ombe wao jike huzaa, asiharibu mimba. Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza. Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi. Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafla. Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako. Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba? Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mipango ya waovu na iwe mbali nami.
Yobu 21:1-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Yasikizeni sana maneno yangu; Jambo hili na liwe faraja yenu. Niacheni, nami pia nitanena; Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki. Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu? Nami kwa nini nisikose kusubiri? Niangalieni, mkastaajabu, Mkaweke mkono kinywani. Hata nikumbukapo nahuzunika, Na utisho wanishika mwilini mwangu. Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu? Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao. Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi. Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba. Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza. Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi. Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafula. Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako. Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba? Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao; Mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
Yobu 21:1-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo Ayubu akajibu: “Yasikilizeni maneno yangu kwa makini; hii na iwe faraja mnayonipa mimi. Nivumilieni ninapozungumza, nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki. “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? Kwa nini nisikose subira? Niangalieni mkastaajabu; mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu. Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa, nao mwili wangu unatetemeka. Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu? Huwaona watoto wao wakithibitika wakiwa wamewazunguka, wazao wao mbele za macho yao. Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu; fimbo ya Mungu haiko juu yao. Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe; ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba. Huwatoa watoto wao nje kama kundi; wadogo wao huchezacheza. Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi, nao huifurahia sauti ya filimbi. Huitumia miaka yao katika mafanikio nao hushuka kaburini kwa amani. Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ Hatuna haja ya kufahamu njia zako. Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? Tutapata faida gani kumwomba? Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe, hivyo najitenga mbali na shauri la waovu.