Yobu 19:21-29
Yobu 19:21-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu, Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa. Mbona ninyi mnaniudhi kama Mungu, Wala hamkutosheka na nyama yangu? Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa! Laiti yangeandikwa kitabuni! Yakachorwa katika mwamba milele, Kwa kalamu ya chuma na risasi. Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu! Kama mkisema, Jinsi tutakavyomwudhi! Kwa kuwa shina la jambo hili limeonekana kwake; Uogopeni upanga; Kwa maana adhabu za upanga zina ghadhabu, Mpate kujua ya kwamba hukumu iko.
Yobu 19:21-29 Biblia Habari Njema (BHN)
Nioneeni huruma, nioneeni huruma enyi rafiki zangu; maana mkono wa Mungu umenifinya. Kwa nini mnanifuatia kama Mungu? Mbona hamtosheki na mwili wangu? “Laiti maneno yangu yangeandikwa! Laiti yangeandikwa kitabuni! Laiti yangechorwa kwa chuma na risasi juu ya jiwe ili yadumu! Najua wazi Mkombozi wangu anaishi, mwishowe yeye atanipa haki yangu hapahapa duniani. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivyo, nitamwona Mungu kwa macho yangu mwenyewe. Mimi mwenyewe nitakutana naye; mimi mwenyewe na si mwingine nitamwona kwa macho. “Nyinyi mwaweza kujisemea: ‘Tutamfuatia namna gani? Tutapataje kwake kisa cha kumshtaki?’ Lakini tahadharini na adhabu. Chuki yenu yaweza kuwaletea kifo! Mnapaswa kujua: Mungu peke yake ndiye hakimu.”
Yobu 19:21-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu, Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa. Mbona ninyi mnaniudhi kama Mungu, Wala hamkutosheka na nyama yangu? Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa! Laiti yangeandikwa kitabuni! Yakachorwa katika mwamba milele, Kwa kalamu ya chuma na risasi. Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu! Kama mkisema, Jinsi tutakavyomwudhi! Kwa kuwa shina la jambo hili limeonekana kwake; Uogopeni upanga; Kwa maana adhabu za upanga zina ghadhabu, Mpate kujua ya kwamba hukumu iko.
Yobu 19:21-29 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma, kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga. Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo? Hamtosheki kamwe na mwili wangu? “Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu, laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu, kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma, au kuyachonga juu ya mwamba milele! Ninajua kwamba Mkombozi wangu yu hai, naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi. Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa, bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu; mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe: mimi, wala si mwingine. Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana! “Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda, maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’ ninyi wenyewe uogopeni upanga, kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga, nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.”