Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 19

19
Bildadi Anena: Mungu Huwaadhibu Waovu
1Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2 # 1 Sam 1:6; Zab 6:2,3 Je! Mtanichukiza nafsi yangu hata lini,
Na kunivunja-vunja kwa maneno?
3Mara kumi hizi mmenishutumu;
Hamwoni haya kunifanyia mambo magumu.
4 # Zab 19:12; Eze 18:4 Ingawaje nimekosa,
Kosa langu hukaa kwangu mwenyewe.
5 # Zab 38:16; Mik 7:8 Kwamba mtajitukuza juu yangu,
Na kunena juu yangu shutumu langu;
6 # Omb 1:13 Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha,
Na kunizingira kwa wavu wake.
7Tazama, nalia, Udhalimu, lakini sisikiwi;
Naulilia msaada, wala hapana hukumu.
8 # Omb 3:7,8 Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita,
Na kutia giza katika mapito yangu.
9Amenivua utukufu wangu,
Na kuiondoa taji kichwani mwangu.
10Amenibomoa pande zote, nami nimetoweka;
Na tumaini langu ameling’oa kama mti.
11 # Kum 32:22 Tena ameziwasha ghadhabu zake juu yangu,
Akanihesabia kuwa mmoja katika watesi wake.
12 # Zab 34:19 Majeshi yake husongea pamoja, na kunipandishia njia yao,
Na kupiga marago kuizunguka hema yangu.
13 # Zab 31:11; Mt 26:56; 2 Tim 4:16 Amewaweka ndugu zangu mbali nami,
Na wanijuao wametengwa nami kabisa.
14Watu wa mbari yangu wamekoma,
Na rafiki zangu niwapendao wamenisahau.
15Wakaao nyumbani mwangu, na vijakazi vyangu, wanihesabu kuwa mgeni;
Mimi ni mgeni machoni pao.
16Namwita mtumishi wangu, wala haniitikii,
Ingawa namsihi kwa kinywa changu.
17Pumzi zangu ni kama za mgeni kwa mke wangu,
Nami ni machukizo kwa ndugu zangu.
18Hata watoto wadogo hunidharau;
Nikiondoka, huninena.
19Wasiri wangu wote wanichukia;
Na hao niliowapenda wamenigeukia.
20Mfupa wangu unagandamana na ngozi yangu na nyama yangu,
Nami nimeokoka na ngozi ya meno yangu tu.
21Nihurumieni, nihurumieni, enyi rafiki zangu,
Kwa maana mkono wa Mungu umenigusa.
22Mbona ninyi mnaniudhi kama Mungu,
Wala hamkutosheka na nyama yangu?
23Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa!
Laiti yangeandikwa kitabuni!
24Yakachorwa katika mwamba milele,
Kwa kalamu ya chuma na risasi.
25Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai,
Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.
26Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi,
Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu;
27Nami nitamwona mimi nafsi yangu,
Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine.#19:27 Au, kama mgeni.
Mtima wangu unazimia ndani yangu!
28Kama mkisema, Jinsi tutakavyomwudhi!
Kwa kuwa shina la jambo hili limeonekana kwake;
29Uogopeni upanga;
Kwa maana adhabu za upanga zina ghadhabu,
Mpate kujua ya kwamba hukumu iko.

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 19: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha