Yeremia 5:12-13
Yeremia 5:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Wamesema uongo juu ya Mwenyezi-Mungu wamesema: “Hatafanya kitu; hatutapatwa na uovu wowote; hatutashambuliwa wala kuona njaa. Manabii si kitu, ni upepo tu; maana neno lake Mungu halimo ndani yao.” Basi hayo na yawapate wao wenyewe!
Yeremia 5:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wamemkataa BWANA, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa; na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa.
Yeremia 5:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wamemkataa BWANA, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa; na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa.
Yeremia 5:12-13 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Wamedanganya kuhusu Mwenyezi Mungu. Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote! Hakuna dhara litakalotupata; kamwe hatutaona upanga wala njaa. Manabii ni upepo tu, wala neno halimo ndani yao; kwa hiyo hayo wayasemayo na yatendeke kwao.”