Isaya 63:7-9
Isaya 63:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu; nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa, kwa sababu ya yote aliyotutendea, wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake, kadiri ya wingi wa fadhili zake. Maana alisema juu yao: “Hakika, hawa ni watu wangu; watoto wangu ambao hawatanidanganya.” Basi yeye akawa Mwokozi wao. Katika taabu zao zote, hakumtuma mjumbe mwingine kuwasaidia, ila yeye mwenyewe alikuja kuwaokoa. kwa upendo na huruma yake aliwakomboa. Aliwabeba na kuwachukua tangu zamani.
Isaya 63:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao. Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.
Isaya 63:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao. Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.
Isaya 63:7-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nitasimulia juu ya wema wa BWANA, kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo BWANA ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi. Alisema, “Hakika wao ni watu wangu, wana ambao hawatanidanganya”; hivyo akawa Mwokozi wao. Katika taabu zao zote naye alitaabika, na malaika wa uso wake akawaokoa. Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa, akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita.