Isa 63
63
Kisasi dhidi ya Edomu
1 #
Isa 34:5-17; Yer 49:7-22; Eze 25:12-14; 35:1-15; Amo 1:11-12; Oba 1-14; Mal 1:2-5 Ni nani huyu atokaye Edomu,
Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra?
Huyu aliye na nguo za fahari,
Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake?
Mimi nisemaye kwa haki,
Hodari wa kuokoa.
2 #
Ufu 19:13
Kwani mavazi yako kuwa mekundu,
Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?
3 #
Omb 1:15; Mal 4:3; Ufu 14:20; 19:13,15 Nalikanyaga shinikizoni peke yangu;
Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami;
Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu,
Naliwaponda kwa ghadhabu yangu;
Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao,
Nami nimezichafua nguo zangu zote.
4Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu,
Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.
5 #
Yn 16:32; Zab 44:3; 98:1; Isa 40:10; 51:9; Isa 59:16 Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia;
Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza;
Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu,
Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
6 #
Ufu 16:6
Nikazikanyaga kabila za watu kwa hasira yangu,
Nikawalevya kwa ghadhabu yangu,
Nami nikaimwaga damu yao chini.
Rehema za Mungu Zakumbukwa
7Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake. 8Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao. 9#Mdo 9:4; 12:11; Kut 14:19; Hos 12:4,5; Mal 3:1; Kum 7:7Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale. 10#Zab 78:8,40; Mdo 7:51; Efe 4:30; Ebr 10:29Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao. 11Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu? 12#Kut 14:21Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kuume wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele? 13Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae? 14Kama ng’ombe washukao bondeni, Roho ya BWANA akawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.
Sala ya Toba
15Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu. 16#Gal 3:28Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako. 17#Zab 119:10; Isa 6:10; Mt 13:15Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako. 18#Dan 8:24Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako. 19Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.
Iliyochaguliwa sasa
Isa 63: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.