Isaya 45:1-3
Isaya 45:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.
Isaya 45:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Koreshi: “Wewe ni mfalme wangu niliyekuteua; mimi naitegemeza nguvu yako ili uyashinde mataifa mbele yako, na kuzivunja nguvu za wafalme. Mimi nayafungua malango ya mji mbele yako, na hakuna lango litakalofungwa. Mimi nitakutangulia, na kuisawazisha milima mbele yako. Nitaivunjavunja milango ya shaba, na kuvikatakata vizuizi vyake vya chuma. Nitakupa hazina zilizofichwa gizani, na mali iliyo mahali pa siri, upate kutambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ninayekuita kwa jina lako.

Isaya 45:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.
Isaya 45:1-3 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
“Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwa mpakwa mafuta wake, Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume kutiisha mataifa mbele yake na kuwavua wafalme silaha zao, kufungua milango mbele yake ili malango yasije yakafungwa: Nitaenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja malango ya shaba na kukatakata mapingo ya chuma. Nitakupa hazina za gizani, mali iliyofichwa mahali pa siri, ili upate kujua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.